Local Bulletins

DCI kufanya uchunguzi wa mauaji ya marafiki wanne walioteweka huko Kitengela.

Picha:Hisani

By Waihenya Isaac,

Kitendawili cha kutoweka kwa watu wanne baada ya kuhudhuria Mkutano wa pamoja Katika kilabu kimoja mjini kitengela huenda kikachukua muda zaidi kuteguliwa.

Hii ni baada ya familia ya Jack Onyango mmoja wa wale waliodaiwa maiti yake ilipakana kando ya mto Mathioya kaunti ya Muranga, kukanusha kuwa maiti hiyo si yake Onyango.

Nduguye mdogo marehemu na mmoja wa wanafamilia amesema kuwa maiti inayodaiwa kuwa ya nduguye sio mwili wa ndugu yao na kwamba ni jukumu la serekali kuwasaidi kuwapata maiti ya Onyango.

Wakti uo huo Inspekta Generali wa polisi Hillary Mutyambai ameitaka idara ya DCI kufanya uchunguzi wa mauaji wa marafiki hao wanne.

Subscribe to eNewsletter