Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
By Samuel Kosgei
Waziri wa afya Mutahi Kagwe ametangaza kuwa taifa hii leo imepoteza watu 11 kutokana na ugonjwa vya Covid-19 ikiwa ndio siku ya kwanza ya mwaka. Idadi hiyo imefikisha walioaga dunia kuwa watu elfu 1,681.
Ameongeza kuwa watu wengine 156 wamekutwa na virusi hivyo baada ya vipimo vya sampuli 4,317 kufanyiwa vipimo na kufikisha visa vyote nchini kuwa 96,614.
Kati ya watu 156 waliopatwa na virusi hivyo 142 ni wakenya ilhali 14 ni raia wa kigeni. 96 ya wagonjwa hao ni wanaume huku 60 wakiwa wanawake. Mdogo ni wa miezi saba huku mkubwa akiwa wa miaka 78.
Kaunti ya Nairobi imeongoza kwa visa 57, Mombasa 23, Busia 15, Kiambu 13 Murang’a 9, Machakos 7, Nakuru 5, Uasin Gishu 4, Kajiado 4, Kitui 4, Nyeri 4, Trans Nzoia 3, Meru 2, Makueni , Kisum, Nandi, Kwale 1 Embu na Homabay ikirekodi kisa moja kila moja.
Watu waliopona hii leo ni watu 65 na kufikisha idadi hiyo kuwa elfu 78,802.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Nairobi Kagwe amesema kuwa wagonjwa 661 wamelazwa katika hospitali mbalimbali huku wengine 2,960 wakilazwa manyumbani.
Wakti uo huo amesema kuwa huenda visa vya corona vikapanda mwezi January kwa kiasi ila akatoa wito kwa wakenya kuzingatia masharti ya wizara afya.
Aidha ametangaza kuwa tayari Kenya imeagiza chanjo ya corona huku akiweka wazi kuwa chanjo hiyo haitakuwa ya lazima. Wakenya wa kwanza kupokezwa chanjo hiyo watakuwa wahdumu wa afya na maafisa wa polisi.