Hali ya jua na ukavu kuzidi kushudiwa Marsabit na sehemu nyingi za nchi
January 7, 2025
By Waihenya Isaac,
Bunge la Kaunti ya Wajir limekuwa la hivi punde kupitisha mswada wa marekebisho wa mwaka wa 2020.
Mswada huo wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa BBI umewasilishwa katika bunge hilo hii leo na kuuidhinisha kwa pamoja na wawakilishi wadi 36 huku mmoja akiupinga.
Kikao cha kujadili mswaada huo pia kilihudhuriwa na Gavana wa kaunti hiyo Mohamed Abdi, huku idadi jumla ya kaunti ambazo zimeidhinisha mswaada huo ifikia 40.
Wawakilishi wadi hao walitaja kuwa bunge hilo limetoa nafasi kwa umma kutoa maoni yao kuhusu mswada huo kufikia hiyo jana.
Aidha wamewataka wananchi kuukubali na kuupitisha mswaada huo utakapowasiliswa kwao wakti wa kura ya maoni.