Local Bulletins

Nitaendelea Kupigania Haki Za Wananchi Wa Tabaka La Chini – Naibu Wa Rais William Ruto.

Naibu Wa Rais William Ruto Alipozuru Kaunti Ya Bomet.
Picha; Hisani

By Samuel Kosgei,

Naibu Wa Rais William Ruto Amekariri Kuwa Ataendelea Kupigania Haki Za Wananchi Wa Tabaka La Chini Kwa Msingi Kuwa Kila Mkenya Ana Haki Ya Kuishi Vizuri Na Kupata Ajira Kama Wakenya Wengine.

Akizungumza Alipozuru Kaunti Ya Bomet Mapema Leo DP Ruto Amesema Kuwa Taifa Hili Halifai Kugawanywa Kwa Msingi Wa Kikabila.

Amepuuzilia Mbali Dhana Kuwa Ni Zamu Ya Makabila Mengine Kutawala Nchi Akisema Kuwa Uchaguzi Ujao Hakutakuwa Ushindani Wa Makabila Bali Zamu Ya Walalahoi Kupata Nafasi Za Ajira.

Naibu Wa Rais William Ruto Pamoja Na Aliyekuwa Gavana Wa Bomet Isaac Rutto Huko Bomet.
Picha; Hisani

Wakti Uo Huo Amemkaribisha Aliyekuwa Gavana Wa Bomet Isaac Rutto Ambaye Amekuwa Mkosoaji Wake Mkubwa Hapo Nyuma. Isaac Ambaye Pia Ni Mwenyekiti Wa Chama Cha Mashinani Amewaomba Wakaazi Wa Kaunti Hiyo Kumrejesha Ugavani Mwaka Wa 2022.

Ruto Alikuwa Ameandamana Na Seneta Wa Bomet Christoper Langat, Senator Kipchumba Murkomen Wa Elgeyo Marakwet Kati Ya Viongozi Wengine.

Subscribe to eNewsletter