Marehemu padre Frank atajwa kama mtu mkarimu aliyependa kusaidia wasiojiweza katika jamii.
January 22, 2025
By Waihenya Isaac,
Akina mama katika maeneo ya Samburu Magharibi wametoa ahadi ya kushirikiana kama jamii kuhakikisha kuwa watoto wote ambao hawajaripoti shuleni kufikia sasa wamerejea.
Wakiongozwa na Mwanaharakati wa kutetea haki za watoto wasichina Daktari Josphine Kulea, akina mama hao wamesema kuwa kwa pamoja watahakikisha kuwa watoto wote wa kaunti hiyo wataendeleza masomo yao katika madarasa ambapo waliachia shule zilipofungwa kwa likizo ndefu mwaka jana kufuatia janga la korona.
Hii ni baada ya akina mama hao kuhudhuria hafla tofauti za hamasisho zilizoandaliwa katika kaunti hiyo kuhusu umuhimu wa elimu.
Inadaiwa kuwa wototo wengi katika kaunti ya Samburu wamesalia nyumbani bila nia ya kurejea shuleni kufuatia utamaduni na mimba za mapema licha ya shule kufunguliwa mwezi mmoja na nusu uliopita.