Local Bulletins

Waziri Yatani Atangaza Ushuru Ulioshushwa Kudhibiti Janga La Corona Kurejea Kuanzia Januari 1, 2021.

Picha;Hisani

Na Adano Sharawe,

Waziri Wa Fedha Ukur Yatani Ametangaza Kuwa Ushuru Ulioshushwa Kudhibiti Janga La Corona Utarejea Katika Hali Ya Kawaida Kuanzia Januari 1, 2021.

Hata Hivyo, Yattani Amesema Wale Wanaopokea Mshahara Wa Chini Ya Sh24, 000 Wataendelea Kufurahia Ushuru Wa Mapatao Uliopunguzwa Kwa Asilimia 100.

Akizungumza Leo Jijini Nairobi, Yattani Amesema Kuwa Hatua Hiyo Imelazimu Kufuatia Kulegezwa Kwa Baadhi Ya Masharti Ya Kuzuia Msambao Wa Virusi Vya Corona Na Kurejelewa Kwa Hali Ya Kawaida Nchini.

Amesema Kuwa Kuanzia Januari 1, 2021, Kiwango Cha Ushuru Kwa Makampuni Kitarejea Kwa Asilimia 30 Kutoka Asilimia 25 Ya Sasa.

Mapato Ya Mtu Binafsi Ya Kiwango Cha Ushuru Wa Ziada (VAT) Yatarudi Kwa Asilimia 16 Kutoka Asilimia 25 Ya Sasa Na Kiwango Cha Ushuru Cha Ongezeko La Thamani Kitarejea Kwa Asilimia 16 Kutoka Asilimia 14 Ya Sasa.

Yattani Amewakumbusha Wakenya Kwamba Serikali Haileti Viwango Vipya Vya Ushuru, Ila Inarejesha Tu Kiwango Cha Ushuru Kilikuwepo Kabla Ya Kuchipuka Kwa Janga Hilo.

Aliongeza Kuwa Serikali Itaendelea Kuimarisha Hatua Chini Ya Programu Ya Kufufua Uchumi (ESP) Kwa Sh58.1 Bilioni Ikiwemo Kazi Mtaani Na Nyingine Kama Njia Ya Kuwaondolea Mzigo Makundi Ya Wasiobahatika Katika Jamii.

Yatani Ameongeza Kuwa Serikali Imeanzisha Mkakati Wa Muda Mrefu Wa Kufufua Uchumi.

Subscribe to eNewsletter