Local Bulletins

Wazazi kaunti nya Marsabit wahitajika kuhakikisha watoto wote wanarejea shuleni

Na Adho Isacko na Mark Dida

Viongozi katika kaunti ya Marsabit wamejitokeza kuwahimiza wazazi kuhakikisha kuwa wanafunzi wao wanarudi shuleni wakati shule zitakapofunguliwa.

Wakiongozwa na naibu kamishna wa marsabit ya kati Patrick Murira, wamesema kuwa jamii ya wafugaji wanajulikana sana kwa kuwaoza watoto wao mapema na hivyo wahakikishe kuwa watoto hao wamerudi shuleni.

Murira amewahimiza wazazi wote ambao muda huu wa kukabiliana na corona wameshirikisha watoto wao kwenye ufugaji au biashara wahakikishe kuwa wamerudi shuleni pindi tu shule zitakapofunguliwa.

Murira ameongeza kuwa yeyote ambaye atapatikana akioza mtoto wake ambaye hajafikisha umri atakamatwa na kuadhibiwa kisheria.  

Kauli hiyo imeshabikiwa na  kaimu chifu wa eneo la karare magdalena ilimo na kuwahimiza wazazi kuweza kuwarudisha nyumbani watoto wote wanaochunga mifugo fora ili waweze kujitayarisha kurudi shuleni.

Wizara ya elimu katika kaunti ya Marsabit kwa ushirikiano na wizara ya afya siku ya Jumatano  zilikagua shule katika kaunti hii kabla ya wanafuzi kurejea shuleni.

Kulingana na mkurungenzi mkuu wa wizara ya elimu katika kaunti ya Marsabit Paul Mwongera bodi ya elimu katika kaunti hii imeshaweka mikakati kambambe ya kupamabana na janaga la korona wakati wanafunzi watakaporejea shuleni. 

Aidha amesema kuwa tayari wizara hiyo imepokea shilingi milioni 26 ili kufanikisha hilo.

Hata hivyo mwongera amesema kuwa mfano wa madawati yatakayotumika upo  katika afisi za wizara hiyo.

Shule za misingi zitapokea madawati 70 huku zile za sekondari zikapokea madawati 50.

Vilevile mwongera  amewataka mafundi wa jimbo hili kutuma maombi ya kupata kandarasi za kutengeneza madawati hayo.

Amewataka wazazi kuhakikisha kuwa watato wanafuata maagizo ya wizara ya afya.

Pia amekariri kuwa shule za mabweni zitakuwa na mahali pa kuwatenga wanafunzi watakaoonyesha dalili za virusi vya korona.

Subscribe to eNewsletter