WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na Jillo Dida
Takriban watu 23 katika wadi ya Ileret, Kaunti ya marsabit wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupind huku wengine 134 wakilazwa hospitalini.
Ugonjwa huo unadaiwa kuzuka mwezi jana na hali imezidi kuwa mbovu zaidi maafa zaidi yakizidi kuripotiwa.
Kulingana na wenyeji wa eneo hilo kijiji cha Ilolo na selicho kilicho katika ufuo wa ziwa Turkana idadi ni kubwa ya walioathirika na kipindupindu kinyume na inavyoelezwa na serikali ya kaunti kwamba ni watu saba pekee ambao wamefariki dunia.
Waziri wa afya Marsabit Jamma Wolde amewaambia wanahabari kuwa watu wawili walifariki hospitalini huku wengine watano wakifariki katika vijiji tofauti akiwemo mtoto mdogo.
Wolde amesema tayari wamethibitisha kuwa maafa ya watu walioripotiwa kufariki yalisababishwa na kipindupindu ugonjwa ambao ulianzia eneo la Bubua nchini Ethiopia kabla ya maambukizi hayo kuvuka hadi Illeret.
Ameongeza kuwa kwa sasa maafisa wa afya wamethibiti hali.
Serikali ya kaunti ya Marsabit inasema kuwa kufikia jana watu 134 walikuwa wameambukizwa kipindupindu na kulazwa katika zahanati za Illeret na Teresagai wakiwa katika hali dhabiti huku wengine wakiruhusiwa kuenda nyumbani.
Dkt Wolde amekiri kuwa kuwa zahanati hizo zina upungufu wa wataalamu ikiwa ni muuguzi mmoja kila moja na hivyo kuchochea serikali ya kaunti kutuma kikiosi cha wataalamu kinachojumuisha wauguzi wanane na wataalamu wa lishe bora pia ikitumwa eneo hilo ili kudhibiti hali japo kwa muda.
Haya yanajiri huku wakaazi wakieleza hisia tofauti kuwa zahanati pekee katika eneo hilo imekabiliwa na changamoto tele za kudhibiti changamoto hizo ikiwemo ukosefu wa wauguzi.
Radio jangwani imebaini kuwa, suala la umbali kati ya watu kuzuia corona imepewa kipaumbele, kwani idadi kubwa ya wagonjwa wanakaa sakafuni palipokuwa mapambajio.
Imesemekana kuwa Ugonjwa huo haswa umewalemea watoto huku visa 52 kati 134 vikiwa watoto wasiozidi umri wa miaka mitano.
Tumebaini pia kuwa idadi kubwa ya wagonjwa wamelazimika kuvuka mpaka na kuingia Ethiopia kutafuta matibabu kwani kituo pekee cha afya katika eneo hilo hakikithi mahitaji ya kudhibiti kipindupindu.
Wakaazi sasa wanataka idara ya huduma za afya katika kaunti kuchukuliwa hatua kutokana na utepetevu katika kukabili changamoto ya ugonjwa huo.