Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
By Adano Sharawe.
Wabunge wameonya kuwa maelfu ya wanafunzi kutoka familia masikini na zisizojiweza pamoja na mayatima ambao hutegemea bursari ya hazina ya CDF kukimu karo huenda wakasalia nyumbani wakati shule zitakapofunguliwa mwezi ujao.
Wabunge wanasema hawajapokea mgao wa fedha za hazina ya ustawi wa maeneobunge yao (NG-CDF) kwa miezi sita katika mwaka huu wa kifedha, hali ambayo sasa inaibua wasiwasi kwamba huenda wanafunzi hao wakakosa karo.
Kulingana na mwenyekiti wa kamati ya NG-CDF, Bunge la Kitaifa Wafula Wamunyinyi amesema hali ni mbaya zaidi kutokana na mlipuko wa janga la Covid-19 ambalo limeathiri uchumi.
Mbunge huyo wa Kanduyi amefichua kuwa hazina ya kitaifa imetoa Sh18 bilioni kati ya bajeti ya Sh41 bilioni kwa mwaka huu wa kifedha.
Hata hivyo, amesema Sh14 bilioni kati ya pesa zilizotolewa zilisambazwa kuziba pengo kwenye bajeti ya mwaka uliopita wa kifedha.