WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Picha; Hisani
Na Adho Isacko,
Huku Ulimwengu Ukiadhimisha Siku Ya Walemavu Hiyo Jana Sherehe Za Kila Mwaka Katika Kaunti Ya Marsabit Hazikufanyika Mwaka Huu Kwa Sababu Ya Mlipuko Wa Covid-19.
Akizungumza Na Radio Jangwani Kwa Njia Ya Simu, Afisa Mkuu Wa Huduma Ya Watu Wenye Ulemavu Katika Kaunti Ya Marsabit Muhammud Kulula Amesema Kuwa, Sherehe Hizo Hazikufanyika Kwa Sababu Ya Idadi Inayoendelea Kuongezeka Ya Covid-19 Katika Kaunti Hii, Ila Wameweza Kuchagua Shule 6 Za Wanafunzi Wanaoishi Na Ulemavu Na Watawasaidia Kwa Kuwapa Barakoa, Vitakasa Na Vifaa Vingine Vya Kujikinga Kutokana Na Maambukizi Ya Covid-19.
Picha; Hisani
Aidha Kulula Amewahimiza Wanaoishi Na Ulemavu Katika Kaunti Hii Kujitokeza Na Kutetea Haki Zao, Kwani Walemavu Wana Ile Haki Ya Asilimia 30 Hasa Wanawake Na Vijana Ya Kujumuishwa Kwenye Kazi Katika Idara Zote Na Hata Serikali Ya Kaunti.
Aidha Kulula Amewahimiza Mashirika Mengine Kujitokeza Na Kuwasaidia Ili Waweze Kusaidia Walemavu Katika Kaunti Hii Ya Marsabit.