Local Bulletins

Seneti Kuandaa Kikao Siku Ya Jumatano Ili Kuamua Namna Hoja Ya Kumwondoa Mamlakani Gavana Sonko Itakavyoshughulikiwa.

 

Picha; Hisani

By Adano Sharawe,

Bunge La Seneti Litaandaa Kikao Siku Ya Jumatano Ili Kuamua Namna Ambavyo Hoja Ya Kumwondoa Mamlakani Gavana Wa Nairobi Mike Sonko Itakavyoshughulikiwa.

Spika Wa Bunge La Seneti Ken Lusaka Ameitisha Kikao Hicho Maalum, Na Amesema Kuwa Maseneta, Ambao Kwa Sasa Wako Likizoni, Watasikiza Malalamishi Yaliyowasilishwa Dhidi Ya Gavana Huyo.

Baadaye Wataamua Iwapo Kesi Ya Gavana Sonko Itashughulikiwa Na Kamati Maalum Ya Bunge La Seneti Au Bunge Lote.

Iwapo Bunge La Seneti Litaamua Kushughulikia Swala Hilo Kupitia Kamati Maalum, Maseneta Watateua Kamati Ambayo Inajumuisha Wanachama 11 Kuchunguza Swala Hilo.

Kamati Hiyo Maalum Itachukuwa Siku Kumi Kufanya Uchunguzi Na Baadaye Kuwasilisha Ripoti Yake Kwa Bunge Hilo.

Picha; Hisani

Bunge Hilo Pia Linaweza Kuchunguza Swala Hilo Kupitia Kwa Vikao Maalum.

Sonko Alifurushwa Afisini Alhamisi Juma Lililopita Katika Hoja Iliyoungwa Mkono Na Wanachama 88 Wa Bunge La Kaunti Hiyo Kati Ya Wanachama 122 Wa Bunge Hilo.

Hata, Hivyo, Sonko Amepinga Matokeo Hayo Akidai Kuwepo Kwa Udanganyifu.

Anadaiwa Kudhihirisha Mienendo Isiyofaa, Kukiuka Katiba Na Kutumia Vibaya Mamlaka.

Aliyekuwa Gavana Wa Kaunti Ya  Kiambu  Ferdinand Waititu Ndie Gavana Wa Pekee Ambaye Kuondolewa Kwake Mamlakani Kumewahi Kufaulu.

Subscribe to eNewsletter