JAMII YA MARSABIT YATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMWA UGONJWA WA MENINGITIS ILI KUPATA MATIBABU MAPEMA.
November 15, 2024
By Adano Sharawe.
Tume Ya Kitaifa Ya Uwiano Na Utangamano NCIC Imetupilia Mbali Mashtaka Dhidi Ya Mbunge Wa Malindi Aisha Jumwa Na Katibu Mkuu Wa Chama Cha ODM Edwin Sifuna Kuhusiana Na Matamshi Yasiyofaa Waliyotoa Hivi Majuzi Wakati Wa Kampeni Za Uchaguzi Mdogo Wa Msambweni.
Kamishna Wa Tume Hiyo Ya NCIC Danvas Makori Amesema Hawatasukuma Tena Mashtaka Dhidi Ya Wawili Hao.
Hii Inajiri Baada Ya Wawili Hao Kuomba Msamaha Hadharani Kwamba Wanajutia Matamshi Yao.
Makori Amesema Wameridhishwa Na Hatua Ya Wanasiasa Hao Wawili Kukiri Makosa Yao Na Kutoa Msamaha Hadharani Kama Ushahidi Wa Nia Yao Ya Mapatano.
Sifuna Anadaiwa Kutoa Matamshi Ya Chuki Tarehe 11 Mwezi Huu Wakati Wa Kampeini Za Uchaguzi Mdogo Wa Eneo Bunge La Msambweni Katika Kaunti Ya Kwale.
Tume Hiyo Inasema Kuwa Matamshi Kama Hayo Yanaweza Kuathiri Jamii Mbali Mbali Zinazoishi Kwa Amani Katika Kaunti Ya Kwale.
Jumwa Anasemekana Kutoa Matamshi Sawa Na Hayo Alipokuwa Akimjibu Sifuna.