Local Bulletins

Naibu rais aunga mkono bunge kuvunjiliwa mbali baada ya barua ya Maraga kwa rais Kenyatta

Na Isaac Waihenya

Naibu wa rais Wiliam Ruto ameunga mkono kauli ya jaji mkuu david maraga ya kumtaka rais Uhuru Kenyatta kuvunja bunge lakitaifa kwa kukosa kupitisha mswada unaohitajika kutekeleza sheria ya uwakilishi sawa wa jinsia.

Akizungumza na viongozi wa kidini kutoka kaunti ya meru katika makao yake ya karen jijini nairobi, naibu wa rais amesema kuwa viongozi wa taifa hili wanafaa kuuondoa ubinafsi na kuwahusisha watu wote katika nyadhifa za uongozi.

Siku ya Jumatatu jaji mkuu David Maraga alimshauri rais Uhuru Kenyatta kuvunja bunge la kitaifa kwa kukosa kupitisha mswada unaohitajika kutekeleza sheria ya uwakilishi sawa wa jinsia.

Kwenye barua kwa rais, Maraga alisema kuwa licha ya mahakama kushauri na kuamrisha bunge mara nne kupitisha mswada huo,bunge hilo limedinda kuupitisha mswada huo kimakusudi.

Subscribe to eNewsletter