Idara ya jinsia kaunti ya Marsabit yalaani kisa cha mauaji ya watoto wawili mapacha katika eneo la Dololo,North Horr.
January 23, 2025
Na Adho Isacko
Watu sita wamewekwa chini ya karantini katika kaunti ndogo ya Moyale. Wanne kati ya sita hao ni madereva wa trela kutoka Addis Ababa huku wengine wawili wakiwa ni kutoka kaunti ya Mombasa eneo la Mtito Andei.
Kulingana na waziri wa afya kaunti ya Marsabit Jama Wolde hadi kufikia Sasa wamepima watu 11 ambao walikua na dalili ya virusi vya corona, sampuli zao kutumwa Nairobi na kudhibiti kuwa hawana virusi vya corona.
Jama amesema kuwa wanaendelea kuwakagua wasafiri ambao wanaingia jimboni.
Katika mipaka ya kenya na Ethiopia ambayo inapakana pia na kaunti jirani ya Wajir wasafiri 140,647 wamekaguliwa na katika eneo ya Merille wasafiri 24,905 wamekaguliwa.
Ameongeza kuwa watu nane pia wamejiweka karantini nyumbani kwao baada ya kusafiri.
Hassan Halakhe ambaye ni mkurugenzi mkuu wa afya ya umma kaunti ya marsabit amewasihi wakazi wa jimbo hili kuzingatia maagizo ya serikali hasa yale ya kusimama umbali wa mita moja au mbili kutoka kwa mtu mwingine na pia ya kutohudhuria sherehe kama kawaida.
Pia amewahimiza wakaazi kunawa mikoni kila baada ya saa chache kwa kutumia maji na sabuni.
Kulingana na ripoti ya hapo awali kuwa hakuna vitanda vya kuweka watu karantini katika eneo la karantini la Marsabit boys.
Mkurugenzi mkuu wa hospitali ya rufaa ya Marsabit Dkt Adano amesema kuwa watafanya mkutano na kuzungumza na kamati tofauti zinahusika ili kuweka vifaa yanayokosekana katika maeneo hayo ya karantini.