Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Picha;Hisani.
Na Samuel Kosgei,
Kinara Wa Chama Cha ODM Raila Odinga Amesema Kuwa Safari Ya Kufanyia Katiba Mageuzi Tayari Imeng’oa Nanga Na Hakuna Cha Kurejea Nyuma Tena Kwenye Mchakato Huo Tena.
Odinga Akizungumza Alipokuwa Akipokezwa Saini Zote Zilizokusanywa Wiki Moja Iliyopita Ili Kufanikisha Marekebisho Ya Katiba Amesema Kuwa Wakti Wa Kukusanywa Kwa Maoni Uliisha Na Kilichosalia Ni Mchuano Wa ‘Ndio Au La.’
Aidha Amepinga Mapendekezo Ya Naibu Wa Rais William Ruto Aliyependekza Kura Hiyo Ya Maoni Ifanyike Sambamba Na Uchaguzi Mkuu.
Amepuuzilia Mbali Suala La Shughuli Hiyo Kuahirishwa Kwa Ajili Ya Virusi Vya Corona Akidai Maisha Hayawezi Kusimama Kwa Ajili Ya Corona.
Picha;Hisani.
Kwa Upande Wake Kiongozi Wa Wengi Bungeni Amos Kimunya Amesifia Mchakato Wa BBI Akisema Kuwa Itasuluhisha Hitaji La Katiba La Kuwa Na Usawa Kijinsia Na Kuepusha Mgogoro Wa Kisheria.
Saini Hizo Zitawasilishwa Kwa Tume Ya Uchaguzi IEBC Ili Kuthibitishwa Kabla Ya Mswada Wa Marekebisho Ya Katiba Mwaka Wa 2020 Kuwasilishwa Katika Mabunge Ya Kaunti.
Mswada Huo Utahitaji Kuidhinishwa Na Angalau Mabunge Ishirini Na Manne Ya Kaunti Kabla Ya Kupelekwa Kwa Bunge La Kitaifa Na Seneti Ili Kuamua Iwapo Wakenya Watashiriki Kura Ya Maamuzi Au La.
Timu Hiyo Ya BBI Imedhibitisha Kupokea Sahihi Milioni 5.2 Kufiikia Mwisho Wa Zoezi Hilo.