Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
By Adano Sharawe & Sanwel Kosgei,
Kenya Inaungana Na Ulimwengu Mzima Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Kupambana Na Ukimwi Duniani Wakati Ambapo Dunia Nzima Inajizatiti Kukabiliana Na Maambukizi Ya Virusi Vya Covid-19.
Wataalam Wanaonya Kuwa Juhudi Zilizoafikiwa Za Kukabiliana Na UKIMWI, Huenda Zikapotea Kwani Nguvu Nyingi Kwa Sasa Zinatumika Katika Vita Dhidi Ya Corona.
Siku Ya Kupambana Na Ukimwi Inapoadhimishwa, Kuna Matumaini Kuhusu Ufanisi Wa Ki-Sayansi Wa Kutafuta Njia Za Kinga Ambazo Zitapunguza Maambukizi Ya Virusi Vya HIV Kwa Asilimia 35.
Taasisi Ya Utafiti Wa Matibabu Humu Nchini (KEMRI), Inashirikiana Na Taasisi Zingine Za Kimataifa Katika Utafiti Wake Kuhusu Pete Ya Dapivirine Ambayo Ndiyo Mbinu Ya Kwanza Ya Kuzuia Maambukizi Ya HIV Kuwahi Kuwasilishwa Kwa Taasisi Za Udhibiti Ili Kuidhinishwa.
Kulingana Na Beatrice Nyagol, Ambaye Ni Mtafiti Katika Taasisi Ya (KEMRI) Iwapo Mbinu Hizo Zitaidhinishwa, Virusi Vya HIV/AIDS Havitaendelea Kuwa Tisho Hapa Nchini Kenya.
Virusi Vya HIV Viliripotiwa Mara Ya Kwanza Nchini Kenya Mwaka Wa 1984 Na Ijapo Hatua Muhimu Zimepigwa Katika Kupunguza Maambukizi Yake, Ugonjwa Wa HIV/AIDS Unaendelea Kuwa Miongoni Mwa Magonjwa Mengine Yanayotatiza Mfumo Wa Afya Humu Nchini Na Uchumi Kwa Ujumla.
Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu Ya Siku Ya Kupambana Na Ukimwi Ni “Komesha HIV Na Covid-19,Tuwajibike”.
Inaaminika Kuwa Wakenya Milioni 1.5 Wanaishi Na Virusi Vya HIV Na Vifo Elfu 20,000 Kuripotiwa Mwaka Jana Pekee.
Kaunti Ambazo Zinaongoza Na Visa Vya Maambukzi Vya HIV Ni Pamoja Na Homa Bay, Siaya, Kisumu, Migori, Kiambu, Kajiado, Mombasa, Kisii, Nairobi, Nakuru, Uasin Gishu Na Kakamega.
Kijinsia Wanawake Wanaongoza Ambapo Kati Ya Visa Milioni 1.5 Idadi Yao Elfu 942,653 Huku Wanaume Wakiwa 565,752