Local Bulletins

IEBC Yazindua Rasmi Zoezi La Kusanifisha Sahihi Za Za BBI.

Picha; Hisani

By Samuel Kosgei,

Tume Huru Ya Uchaguzi Na Mipaka IEBC Hii Leo Inazindua Rasmi Zoezi Zima La Kusanifisha Sahihi Za Mpango Wa BBI Ambazo Ziliwasilishwa Kwao Na Kundi Linalounga Mkono Mchakato Huo.

Uzinduzi Wa Zoezi Hilo Linafanyika Katika Ukumbi Wa Bomas Of Kenya Jijini Nairobi Ukiongozwa Na Mwenyekiti Wa Tume Hiyo Wafula Chebukati Na Makamishna Wa Tume Hiyo Huku Makarani 400 Wakipewa Kazi Ya Kusanifisha Sahihi.

Makarani Wa IEBC Watakaosanifisha Sahihi Za BBI.
Picha; Hisani

Mrengo Unaotaka Katiba Kufanyiwa Mabadiliko Uliwasilisha Sahihi Zaidi Ya Milioni Nne Katika  Ofisi Za Tume Ya IEBC Iweze Kutahminiwa Kabla Ya Mswada Huo Kutumwa Kwa Katika Mabunge Ya Kaunti Ijadiliwe, Kupitishwa Au Kuangushwa Kama Ulivyofanyika Katika Mswada Wa Punguza Mzigo Uliofadhiliwa Na Chama Third Way Alliance Mwaka Jana.

Mswada Huo Unahitaji Uungwaji Mkono Wa Kaunti 24 Ili Ivuke Hatua Nyingine.

Subscribe to eNewsletter