Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
By Samuel Kosgei
TUME huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imetenga February 18, 2021 kuwa siku ya uchaguzi mdogo wa kaunti ya Nairobi kumtafuta gavana atakayechukua nafasi ilioachwa wazi na Mike Sonko.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, kupitia gazeti rasmi la serikali ameshauri vyama vyote vya kisiasa vinavyopania kuwania ugavana Nairobi kuwasilisha majina ya watakaowania mchujo wa vyama kabla Jumatatu, December 28, 2020.
Wafanyakazi wa umma wanaopania kuwania nafasi wanafaa kujiuzulu kutoka ofisi hizo za umma katika kipindi cha siku saba tangu nafasi hiyo kutangazwa kuwa wazi.
Uteuzi wa vyama unafaa kufanyika, January 18 na January 19, 2021.
IEBC aidha imesema kuwa kipindi cha kampeni itaanza January 18, na kumalizika February 15, 2021.
Jumatatu spika wa bunge la Nairobi Benson Mutura aliapishwa kushikilia kiti hicho kwa kipindi cha siku 60 kikaimu.