Vijana wazidi kutiwa shime kupigania haki zao nchini.
January 21, 2025
Na Waihenya Isaac,
Ofisi Kuu Inayoshughulikia Mchakato Wa BBI Pamoja Na Wanaounga Mkono Suala Hilo Nchini Leo Wamekabidhi Tume Huru Ya Uchaguzi Na Mipaka IEBC Sahihi Za BBI Zaidi Ya Milioni Tatu Walizokusanya Wakti Wa Zoezi La Ukusanyaji Sahihi.
Timu Hiyo Inayoongozwa Na Kinara Wa Wachache Bungeni Junet Mohammed Na Mwenzake Aliyekuwa Mbunge Wa Dagoreti Dennis Waweru Ilisema Kuwa Tayari Safari Yao Imengoa Nanga Na Hakuna Kusimama Tena.
Akizungumza Baada Ya Kupokea Sahihi Hizo,Mwenyekiti Wa Tume Ya IEBC Wafula Chebukati Amesema Kuwa Shughuli Ya Kuzikagua Sahihi Hizo Itaanza Baada Ya Tume Hiyo Kukabidhiwa Fedha Za Kuiendeleza.
Kulingana Na Chebukati Tume Hiyo Itatekeleza Majukumu Yake Kwa Wakti Ufaao.
Mwanzo Sahihi Milioni 5.2 Zilikuwa Zimekusanywa Ila Zikapungua Hadi Karibia Milioni Tatu Baada Ya Kufanyia Dhibitisho.
Endapo IEBC Itapitisha Sahihi Hizo Basi Mswada Wa Marekebisho Ya Katiba Utawasilishwa Katika Mabunge Ya Kaunti Kote Nchini Kupitishwa Au Kukataliwa.
Iwapo Itafaulu Kupitishwa Na Mabunge 24 Basi Utapelekwa Katika Bunge La Seneti Ya Bunge La Kitaifa Ili Kuidhinishwa.