Jimbo katoliki la Marsabit laadhimisha miaka 60 ya kueneza Injili.
November 23, 2024
Na Jillo Dida Jillo
Ngamia katika maeneo kadha jimboni Marsabit wameadhirika na ugonjwa wa mafua na kuonyesha dalili nyingine ambazo wakaazi wameeleza sintomfahamu kuzihusu.
Visa vya ngamia kufariki katika jimbo la marsabit viliripotiwa tangu mwezi Januari mwaka huu baada ya mlipuko wa virusi vya mers-cov kwa kiengereza middle east respiratory syndrome coronavirus, virusi vinayoaamika kuwa na uhusiano wa kifamilia na virusi vya corona ambavyo kwa sasa vimetikisa dunia mzima.
Serikali ya kaunti ilitangaza kuwa familia ya virusi vya corona kwa jina mers-cov vilipatikana katika kaunti hii japo wizara ya afya ilidinda kutoa mwanga zaidi kwa madai kuwa bado wanafanya utafiti kuhusu ugonjwa huo kwa ushirikiano na chuo kikuu cha washington kutoka marekani.
Kulingana na Waziri wa kilimo na ufugaji kaunti ya marsabit Wario Sori ni kwamba virusi hivyo vinaweza kusambazwa kutoka kwa mifugo hadi kwa binaadamu madai ambayo imewapa wasiwasi wafugaji katika kaunti ya marsabit hususan wa ngamia.
Wizara ya kilimo na ufugaji kaunti ya marsabit ilieleza kuwa vita dhidi ya virusi vya corona vimepewa kipaumbele na wizara ya afya huku hatari inayowakodolea macho wafugaji ikionekana kupuuzwa.
Ugonjwa huo umeripotiwa kuaadhiri mifugo katika maeneo ya Badha hurri, Bubisa, Burgabo, yaa galbo, yaa gara, Tulu Dimtu na Meikona katika kaunti ndogo ya North Horr na vile vile hivi maajuzi maeneo ya Watiti na Nana katika kaunti ndogo ya Moyale.
Mifugo ilioadhirika zaidi ni ngamia kwani wafugaji kwa sasa wamekadiria hasara kubwa ikizingatiwa kuwa ngamia ndio kitega uchumi pekee haswa katika eneo bunge la North Horr na Laisamis.
Aidha swala la umbali wa mji wa marsabit ambapo uratibu wa huduma za wafugaji hutolewa pia limetajwa kama changamoto kuu kwa wafugaji hao.
Kulingana na Tumal Orto mkaazi wa Maikona na mfugaji wa ngamia ni kuwa ngamia wameonyesha dalili za kukohoa, mafua na makamasi na pia uvimbe shingoni kabla ya dalili hizo kuzidi na kusababisha ngamia kufa.
Kati ya wafugaji tuliozungumza nao ni kwamba ugonjwa huo umesambaa kwa kasi na kitendawili kwao ni kuwa dalili hizo zinatofautiana, wengi wakisema kuwa wanaoadhirika zaidi ni watoto wa ngamia wanaojulikana kama nirigi.
Viyeyushi, barakoa, kukaa umbali wa mita moja au zaidi na maagizo mengine ya wizara ya afya kuhusu kukabili kusambaa kwa virusi vya corona vimesalia kuwa historia magazetini, radioni na gumzo la mitaani kwa wafugaji.
Wamesema kuwa wamepokea habari kuhusu virusi vya corona ila imekuwa vigumu kwao kuzingatia maagizo hayo kwani mazingira wanayoishi hayawaruhusu.
Sasa wanasema ujio wa mercov umefanya hali ya maisha kuwa ngumu zaidi kwa wafugaji wa hapa jimboni.
Pamoja na hayo kumekuwa na laalama kutoka kwa wafugaji wa ngombe katika eneo la badha hurri wakidai kuwa ngombe wanaugua ungonjwa wa ngozi ambao wataalamu waliutaja kama ugonjwa wa mapele ngozi yaani lampy skin disease(LSD).
Bathi ya athari za ugonjwa wa mapele ngozi (lumpy skin disease, LSD) imetanjwa kuwa.
1. Hasara za kiuchumi hasa kutokana kushuka kwa bei ya ngozi.
2. Kupunguza uzalishaji wa maziwa
3. Utatiza ukuaji wa mifugo
4. Kuavia mimba
5. Na pia kupelekea kifo
Ugonjwa huu pia huenezwa na virusi wajulikanao kwa jina la kitaalamu kama lumpy skin disease virus waliopo kwenye familia ya poxviridae.
Wizara ya kilimo na ufugaji kaunti ya marsabit imedhibitisha kuwa ugonjwa huo umeadhiri mifugo jimboni haswa katika kaunti ndogo za Laisamis, North horr na Moyale.