KNUT Marsabit yakanusha madai ya walimu kunyimwa huduma za matibabu kutokana na kucheleweshwa kwa fedha na TSC
February 3, 2025
Na Waihenya Isaac
MAHAKANI BY WAIHENYA 4PM……………….
Mshukiwa kwenye mauaji ya Kevin Omwenga,Chris Obure amepata pigo baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kutaka kufanywa kuwa shahidi badala ya kuwa mshukiwa kwenye mauji hayo.
Akitoa uamuzi kwenye kesi hiyo Jaji Mumbi Ngugi ameamuru kuwa ombi la mshukiwa huyo halina misingi na Kuwa mahakama haina ruhusa ya kuuamulia upade wa mashtaka kuhusu ni nani anafaa kuwa mshukiwa au shahidi.
Aidha Mahakama hiyo imesema kuwa uamuzi kuhusiana na swala hilo utatolewa wakati wa kuendelea kwa kesi hiyo kwa kuzingatia ushahidi utakaowasilishwa.
Obure alikuwa amekataa kula kiapo kwenye kesi hiyo na badala yake kutaka abadilishwe na kuwa shahidi kwenye mauaji hayo yaliyotokea tarehe 21 mwezi Agosti mwaka huu katika eneo la kilmani jijini Nairobi.