Local Bulletins

Wagonjwa 11,324 Wamepona Ugonjwa Wa Korona Huku Idadi  Ya Walipona Yafika  67,788.

Picha;Hisani

By Waihenya Isaac

Kenya Imetangaza Idadi Kubwa Zaidi Ya Wagonjwa Waliopona Virusi Vya Korona Kwa Siku Tangu Kisa Cha Kwanza Cha Korona Kuripotiwa Humu Nchini Mapema Mwezi Machi Mwaka Huu.

Kwenye Taarifa Ya Kila Siku Kuhusu Hali Ya Maambukizi Nchini,Katibu Wa Utawala Katika Wizara Ya Afya Daktari Rashid Aman Ametaja Kuwa Wagonjwa 11,324 Wamepona Ugonjwa Huo Huku Idadi  Ya Walipona Virusi Vya Korona Nchini Ikiwa  67,788.

Aidha Watu Wengine 1,253 Wamepatikana Na Virusi Hiyo Na Kufikisha Jumla Ya Visa Vya Ugonjwa Huo Nchini Kuwa 86,383.

Visa Hivyo Vipya Ni Kutoka Kwa Sampuli 10,170 Zilizopimwa Kwa Saa 24 Zilizopita Na Kufikisha Jumla Ya Sampuli Zilizopimwa  Nchini Kuwa  911,598.

Picha;Hisani

Wagonjwa 747 Ni Wanaume Ilhali 506 Ni Wanawake Huku Mgonjwa Wa Umri Wa Chini  Akiwa  Mtoto Wa Umri Wa Mwaka Mmoja Ilhali Wa Umri Wa Juu Ana Miaka 88 .

Kadhalika Watu Wengine 16 Wameaga Dunia Kutokana Na Virusi  Vya Korona Na  Kufikisha  Idadi Ya Walioaga Nchini Kuwa 1500.

Kaunti Ya Nairobi Inazidi Kuongoza Kwa Visa 326, Mombasa 143, Kilifi 105, Kiambu 86, Murang’a 67, Meru 45, Kirinyaga 43, Makueni 36, Migori 35, Embu 34, Laikipia 32, Nakuru 26, Machakos 25, Kitui 24, Na Taita Taveta 20,

Bungoma 19, Siaya 18, Lamu 17, Nyeri 17, Uasin Gishu 14, Kajiado 13, Garissa 13, Nnandi 12, Kisumu 12, Tharaka Nithi 12, Bomet 11, Homa Bay 10, Busia 7, Kakamega 6, Kwale 5.

Subscribe to eNewsletter