KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Adano Sharawe.
Watu 2 wameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakipata majeraha mbalimbali baada ya gari dogo kuhusika kwenye ajali mapema leo katika barabara ya Marsabit-North Horr.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Dadhach Boshe kilomita chache kutoka hapa mjini Marsabit.
Gari hilo lilikuwa safarini likitokea North Horr.
Inasemekana kuwa gari hilo aina ya Land cruiser lilikuwa katika mteremko wakati lilikosa mwelekeo na kuacha barabara kabla ya kubingiria mara kadhaa na kuanguka.
Mmoja wa waathiriwa ni mtahiniwa wa kidato cha nne aliyekamilisha kuandika mtihani wake jana.
Wa pili ni msaidizi wa dereva ambao wote walifariki papo hapo.
Manusura akiwemo dereva wanapokea matibabu katika hospitali ya rufaa ya Marsabit.
Mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo huenda ilichangia ajali hiyo kutokea.