WAUGUZI KATIKA KAUNTI YA MARSABIT WAMEAPA KUENDELEA NA MGOMO WAO HADI PALE SERIKALI YA KAUNTI YA MARSABIT ITAKAPOSHUGHULIKIA MATAKWA YAO YOTE.
September 19, 2024
Na MACHUKI DENSON
Takriban watu kumi na mmoja walifariki katika visa vya ajali kila siku mwezi Desemba mwaka jana. Haya ni kw amujibu wa mamlaka ya uchukuzi na usalama wa barababarani nchini NTSA.
Kulingan a na NTSA mwezi huo wa disemba mwaka jana jumla ya watu 342 walifariki kutokana na ajali za barabarani.
Kwenye kikao na wanahabari hii leo NTSA kwa ushirikiano wa idara ya polisi wameonya kuongeza nguvu katika kuyakagua magari yote ya uchukuzi wa umma barabarani wakati huu dunia nzima inaingia katika kipindi cha krisimasi.
NTSA pamoja na polisi wamewataka madereva kupanga safari zao mapema na kuhakikisha magari yao yanaafikia matakwa ya barabarani ili kuepuka kukabiliwa kisheria.
Takwimu za NTSA zinaonyesha kwamba kufikia sasa tangu mwezi Januari mwaka huu takriban watu 3,388 wamepoteza maisha yao kupitia ajali za barabarani.
NTSA inasema hii ni idadi iliyoongezeka ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana. Kulingana na NTSA asilimia 93 ya ajali zinatokana na makosa ya kibinadamu ikiwemo kupoteza mwelekeo, mwendo wa kasi ya juu, ukosefu wa nidhamu barabarani na kubeba wat kupita kiasi.
NTSA pamoja na polisi wamewaomba madereva kumakinika barabaranai hata wakati wakiendeleza kampeni ya usafiri salama na kufanya ukaguzi wa magari ya umma.
Polisi pamoja na NTSA wameonya kwamba iwapo gari moja la uchukuzi litagundulika kuhitilafiana na kithibiti mwendo basi kampuni nzima italazimika kusitisha kazi zake muda ukaguzi wa magari yote ya kampuni ukifanywa.
Aidha ukaguzi wa ghafla unatarajiwa kufanyika kuanzia leo usiku na mchana sehemu mbali mbali kuhakikisha wote wanaoendesha magari wana leseni au magari yao yapo salama kwa barabara.