Loading Now

Highlights

Baadhi ya maeneo kaunti ya Marsabit kuendelea kupokea mvua katika kipindi cha siku saba zijazo

Na Sabalua Moses

Utabiri wa hali ya hewa kaunti ya Marsabit katika siku 7 zijazo kuanzia leo tarehe 14 mpaka 20 unaashiria kuwa kutakuwa na ongezeko katika kiwango cha mvua katika sehemu tofauti za jimbo la Marsabit.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa kaunti ya Marsabit John Nguyo, maeneo ya Sololo, Moyale, Golbo, Obbu na Butiye yatapokea mvua kati ya milimita 56 hadi 143.

Maeneo ya Uran na baadhi ya sehemu za Maikona yanatarajiwa kupokea mvua ya wastani ya millimita 28 hadi 56.

Maeneo ya Marsabit Central, Saku, Sagante Jaldesa, Turbi na Kargi yanatarajiwa kupokea mvua kiwango cha chini cha kati ya milimita 1-28.

Hata hivyo maeneo ya North Horr, Dukana, Illeret, Loiyangalani, Laisamis, Korr|Ngurnit yanatarajiwa kushuhudia hali ya ukavu.

Aidha, baadhi ya maeneo jimboni yanatarajiwa kupokea upepo wastani hadi mkali kutoka kusini hadi kusini-mashariki.

Hata hivyo, maeneo mengi ya Loyangalani yanatarajiwa kukumbwa na upepo mkali sana.

Idara hiyo imetoa tahadhari kwa wananchi wanaoishi katika maeneo yatakayoshuhudia mvua ikiwataka kuepuka maeneo hatarishi.

Vile vile madereva wametakiwa kuwa waagalifu barabarani na kutumia njia mbadala pale itakapohitajika.

Post Comment