Highlights

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Ukur Yatani, awahimiza vijana kuchagua viongozi watakaosaidia kutatua changamoto zinazowakabili kila siku.

NA NYABANDE ORWA

Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Ukur Yatani, amewahimiza vijana kujitokeza na kuchagua viongozi watakaosaidia kutatua changamoto zinazowakabili kila siku. Akizungumza wakati wa harambee ya kusaidia kundi la vijana katika eneo bunge la Saku, Yatani amesema kuwa njia pekee ya kuboresha maisha ya vijana ni kuchagua viongozi waadilifu wanaoweka miradi ya kuwasaidia kiuchumi na kijamii.

Kiongozi huyo, ambaye pia alikuwa gavana wa kwanza wa Kaunti ya Marsabit, ameikosoa serikali ya sasa ya kaunti kwa kushindwa kuanzisha miradi ya kuwasaidia wananchi licha ya kupokea fedha nyingi kutoka kwa serikali kuu. Ameongeza kuwa huduma nyingi zimezorota, akitaja sekta ya afya kuwa miongoni mwa zilizoshindwa kutoa huduma bora.

Wakati huo huo, Yatani amewataka wananchi kuacha kuchagua viongozi kwa misingi ya kikabila na badala yake kuangalia utendakazi wao.

Kwa upande wake, kiongozi wa vijana wa kikundi cha waendesha boda boda cha Sogam, Guyo Duba, ametoa wito kwa viongozi wa Kaunti ya Marsabit kuiga mfano wa Ukur Yatani katika kuwaunga mkono vijana ili waweze kujiimarisha kiuchumi kupitia vikundi vyao.

Duba amesema fedha zilizokusanywa katika harambee hiyo zitasaidia kuanzisha mradi wa kilimo, ikiwemo ufugaji wa kuku na upanzi wa nyasi, ili kuongeza kipato cha vijana hao. Aidha, amewahimiza vijana kujitokeza na kudai haki zao kwa kuchagua viongozi bora ili kusonga mbele kiuchumi.

Katika harambee hiyo, jumla ya shilingi milioni 2.46 zilikusanywa.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment