Nyingi ya shule Marsabit kutoa mafunzo ya STEM na Sayansi ya Kijamii huku Sanaa na Spoti ikitajwa kuwa na changamoto ya muundo msingi.
NA SAMUEL KOSGEI
Shule nyingi kwenye gredi ya 10 hadi 12 katika kaunti ya Marsabit zitatoa masomo ya CBE katika njia mbili ambayo ni (STEM) na Sayansi ya Kijamii yaani Social Sciences.
Katibu wa chama cha walimu wa shule za sekondari KUPPET Sarr Galgalo, ameambia shajara kuwa shule nyingi hapa Marsabit hazina muundo msingi nzuri ya kutoa mafunzo ya Sanaa na Sayansi ya michezo kama inavyotakiwa na idara ya elimu nchini.
Anasema kutokana na changamoto hiyo itakuwa vigumu kwa shule nyingi humu jimboni kusomesha somo la Sanaa na sayansi ya Michezo.
STEM inajumuisha masomo kama vile Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.
Hata hivyo anasema kuwa wizara ya elimu imewakikishia kuwa matayarisho yote yako vizuri kwa ajili ya kupokea wanafunzi wa gredi ya 10 January mwakani.



Post Comment