Idara ya kukusanya ushuru Marsabit yatakiwa kuziba mianya ya wizi ili kufikisha shabaha yao.
February 28, 2025
NA SAMUEL KOSGEI
Mwenyekiti wa bajeti katika bunge la kaunti ya Marsabit Daud Tomasot amesema kuwa kamati yake imetenga shilingi milioni 700 katika mwaka wa kifedha 2024/25 kwa ajili ya kulipa madeni ya wakenya waliotoa huduma yoyote wa serikali ya kaunti.
Akizungumza na idhaa hii kwenye kipindi cha Amkia Jangwani asubuhi ya leo, Tomasot amesema kuwa deni lote ambalo halijalipwa kwa wakenya waliohudumia kaunti kulingana na kamati maalum iliyobuniwa kufuatilia madeni hayo ni shilingi bilioni 1.5
Katika bajeti ya ziada walioidhinisha siku ya jumatano sh. 190m ilitegwa kwa ajili ya kupunguza madeni hayo.
Wakati huo Tomasot amesema kuwa bado serikali ya Marsabit kwa upana inategemea sana mgao wa serikali kuu kutatua mahitaji ya pesa.
Anasema kuwa licha ya idara ya fedha kuweka shabaha ya kukusanya shilingi 110m ktk kaunti ya Marsabit bado inakuwa vigumu kufikisha lengo hilo.
Ameitaka idara ya kukusanya ushuru jimboni kutia juhudi na kukusanya ushuru utakaofikisha shabaha wanayolenga kwa kufanya zoezi hilo kupitia njia ya kidijitali utakaopunguza wizi wa pesa za umma.