Idara ya kukusanya ushuru Marsabit yatakiwa kuziba mianya ya wizi ili kufikisha shabaha yao.
February 28, 2025
Huku waumini wa dini ya kiislamu wakijianda kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan wito wa Amani na upendo umetolewa miongoni mwa waumini hao.
Akiongea na shajara ya Radio Jangwani imam wa msikiti wa jamia mjini Marsabit sheikh Mohamed Noor amewataka waumini wa dini hiyo kutokufuata maneno ya wanasiasa yanayoweza kutibua amani miongoni mwa wananchi.
Wakati uo huo Sheikh amelalamikia hali mbaya ya kiuchumi sasa akiiomba serikali na mashirika yasio ya kiserikali kuingilia kati na kusaidia kuwapa wananchi maji na bidhaa za vyakula haswa ikizingatiwa kuwa kunao wasio na uwezo huo.
Haya yanajiri huku wakenya wengi wakilalamikia hali mbaya ya uchumi unaoathiri hali ya lishe na biashara.
Wakati uohuo amewarai wakaazi kukumbatia msamaha kati yao kama njia moja ya kuimarisha umoja baina ya wakaazi.
Haya yanajiri huku wakenya wengi wakilalama hali mbaya ya uchumi unaoadhiri hali ya lishe na biashara.