Local Bulletins

Maafisa wa polisi waliohudumu za zaidi ya miaka mitano katika eneo moja wanafaa kuhamishwa. – Asema mwanaharakati Fredrick Ochieng.

Na JB Nateleng,

Ili kushinda vita vya dhidi ya matumizi ya mihadarati katika kaunti ya Marsabit ni sharti serekali iweze kuwahamisha maafisaa ambao wamehudumu katika eneo moja kwa zaidi ya miaka 5 au zaidi.

Haya yamekaririwa na mwanaharakati anayepambana na matumizi ya mihadarati na dawa za kulevya hapa jimboni Fredrick Ochieng.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani kwa njia ya kipekee,Ochieng amesema kuwa serekali inafaa kuwahamisha maafisa wote ambao wamehudumu katika kaunti ya Marsabit kwa zaidi ya miaka 4 na kuwaleta wapya ambao watasaidia katika kupambana na matumizi ya mihadarati, kwani waliohudumu kwa miaka mingi wanalegeza Kamba katika vita hivyo.

Ochieng amesisitiza kwamba ni sharti walanguzi wa mihadarati wakamatwe na kushtakiwa kulingana na sheria.

Mwanaharakati huyu ameunga mkono hatua ya idara ya usalama kuendeleza msako dhidi ya mihadarati na pombe haramu ambayo ametaja kwamba imeadhiri vijana pakubwa.

Aidha Ochieng amewataka vijana kukumbatia mafunzo ya vyuo vya anuwai ili kujipusha na maovu au hata utumizi wa mihadarati.

Hata hivo Ochieng amewataka wawakilishi wadi katika Kaunti ya Marsabit kuyapa masuala ya vijana kipaumbele ili kuwaokoa katika jinamizi la dawa za kulevya.

Subscribe to eNewsletter