Watu 25 ikiwemo watoto 6 waendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe,Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia.
February 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Watu 25 ikiwemo watoto 6 wanaendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe, eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia mnamo siku ya jumamosi wiki jana.
Kwa mijibu muuguzi katika zahanati ya Kamboe John Lenareiyo ambaye ameongea na Shajara Ya Radio Jangwani kwa njia ya simu ni kuwa wanakijiji katika Manyatta ya Lengorino wamewarifu wahudumu wa afya ambao wamezuru kijiji hicho kuwa wakaazi hao walikula nyama iliyoletwa na wafugaji waliotoka FORA mnamo siku ya jumamosi.
Lenareiyo amesema kuwa kwa sasa waadhirika wako katika hali shwari baada ya kupokea matibabu.
Lenareiyo ametoa wito kwa wananchi wa eneo hilo kutokula nyama yeyeote haswa haswa kutoka kwa mifugo waliofarika kwani hilo linaweza hatarisha afya yao.