Watu 25 ikiwemo watoto 6 waendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe,Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia.
February 25, 2025
Na Samuel kosgei
Kama juhudi za kusaidia katika kupunguza au kumaliza maambukizi ya ugonjwa wa Kalaazar katika eneo la Loglogo, mashirika yasiyo ya kiserikali yametolewa wito kuingilia kati na kusaidia katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo sumbufu.
Katibu Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la kuimarisha maisha ya wafugaji la REPAL Eddy Lemoile amesema kuwa ni kupitia kuja pamoja kwa serikali ya kaunti, ya kitaifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ndipo vita hivyo vitafanikiwa.
Ameyasema hayo katika kituo cha afya cha Loglogo wakati shirika hilo lilipotoa msaada wa dawa za kunyunyiza kuua wadudu wa sand fly wanaotajwa kuambukiza Kalaazar.
Dawa hizo anasema itasaidia katika kunyunyizia nyumba zaidi ya 350 kati wadi ya Loglogo.
Wakaazi wa eneo hilo wamekariri haja ya mashirika kama REPAL kujitokeza na kusaidia kutokomeza kero la Kalaazar na pia mti wa mathenge anayodai inatoa fursa nzuri kwa wadudu hao kuzaana Zaidi.