Watu 25 ikiwemo watoto 6 waendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe,Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia.
February 25, 2025
Na Caroline Waforo,
Visa vya wazazi kutelekeza majukumu ya ulezi vimeongezeka katika kaunti ya Marsabit.
Hii ni baada ya kusitishwa kwa misaada ya Marekani kupitia shirika la USAID majuma kadhaa yaliyopita na rais wa sasa wa Marekani Donald Trump pindi tu alipochukua usukani.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani afisini mwake afisa wa watoto katika eneo bunge la Saku, Mukanzi Leakay amedokeza kuwa kaunti ya Marsabit ni mojawepo ya kaunti zilizokuwa zikinufaika zaidi na misaada hiyo hivyo basi kuathirika pakubwa baada ya misaada kusitishwa.
Aidha Mukanzi amewataka wazazi kutafuta njia mbadala za kujikimu kimaisha ili kupata namna za kuwalea na kuwatunza wanao.
Vilevile afisa huyu wa watoto amedokeza kuwa wanawasaidia watoto waliotelekezwa baada ya kufanya uchunguzi na kubaini fika kuwa wazazi hawawezi kumudu hata karo ya wanao.
Na huku watoto wakiwa nyumbani kwa likizo fupi ya katikati mwa muhula huu wa kwanza Mukanzi amewataka wazazi kuwajibika katika malezi haswa kuhusu utumizi wa mitandao miongoni watoto.
Tayari wanafunzi washaanza likizo hii fupi leo Jumanne.