Local Bulletins

Wakaazi mjini Marsabit watoa hisia kinzani kuhusiana na ‘Handisheki’ kati ya ya rais William Ruto na kinara wa Azimio Raila Odinga…..

Na Joesph Muchai,

Wakaazi mjini Marsabit wametia doa muungano baina ya rais William Ruto na aliyekuwa waziri mkuu ambaye pia ni kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga.

Baadhi ya waliozungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani wameonyesha wasiwasi wao kuhusiana na muungano huo wakisema kuwa hakuna suluhu litakaloundwa kwenye muungano huo.

Wanahoji kuwa Raila Odinga anafaa zaidi kuwa upande wa upinzani ili kulainisha mambo yanayowaddhiri Wakenya.

Kauli zapo zinajiri siku moja tuu baada ya rais William Ruto kusema kuwa atafanya kazi kwa ushirikiano na kinara huyo wa chama cha chungwa haswa baada yake kupoteza kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa muungano wa Afrika AUC.

Subscribe to eNewsletter