Watu 25 ikiwemo watoto 6 waendelea kupokea matibabu katika eneo la Kamboe,Marsabit baada ya kudaiwa kula mzoga wa ngamia.
February 25, 2025
Na JB Nateleng,
Tunahitaji mtaalamu atakayewafunza watot wetu kuhusu madhara ya mihadarati shuleni. Haya ni kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya SKM Kame Koto.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, mwalimu Kame amesema kuwa ipo haja ya wanafunzi kufunzwa kuhusiana na madhara ya mihadarati ili kuwawezesha kuchukua tahadhari inayofaa mapema.
Mwalimu Kame ameelezea kwamba baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakidanganya kuhusu utumizi wa dawa ya kulevya aina ya ORS huku akiitaka serekali kuweza kuchunguza zaidi na kuwakamata wahusika.
Aidha Mwalimu Kame amewanyoshea kidole cha lawama wafanyibiashara wanaowauzia watoto dawa za kulevya akiwataja kama watu wasiojali kizazi kijacho.
Kaluli ya Mwalimu kame inajiri huku idara ya usalama kaunti ya Marsabit ikiendeleza msako dhidi ya mihadarati na pombe haramu.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo ni kuwa msako huo utaendelea huku akitoa onyo kwa walanguzi wa dawa za kulevya pamoja na wale wanaojishughulisha na biashara ya pombe haramu kuasi biashara hiyo mapema iwezekanavyo au wakabiliwe kisheria.