Local Bulletins

Mwenyekiti wa NCCK, tawi la Marsabit mchungaji Saido Diba, awaraia wanaMarsabit kuasi mila potovu na zilizopitwa na muda……

NA ISAAC WAIHENYA

Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wameshauriwa kuasi mila potovu na zilizopitwa na muda na badala yake kuangazia mila zinazofaa.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa baraza la makanisa mbalimbali nchini NCCK, tawi la Marsabit mchungaji Saido Diba, ni kuwa ni jambo la kuhuzunisha mno kuona kwamba bado kuna jamii ambazo zimeshikilia mila zilizopitwa na muda ambazo zinahujumu haki za binadamu.

Akionekana kurejelea kisa cha majuma machache yaliyopita ambapo watoto mapacha waliuwawa katika eneo la Dololo Boji kaunti ndogo ya Dukana, mchungaji Diba amekashifu swala hilo huku akilitaja kama linalohujumu haki za binadamu huku akiwataka wahusika kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili wawe funzo kwa wanaoendeleza mila zananyanyasa wanajamii.

Hata hivyo mchungaji Saido pia amekemea mila ya wizi wa mifugo ambayo pia anataja kuwa imepitwa na muda.

Hata hivyo mchungaji Diba amewarai wazazi kuwa makini na wanachofanya wanao kwenye mitandao ya kujamii ili kuwazuia dhidi ya kujiingiza katika maswala yanayoweza kuwapotosha kimaadili.

Subscribe to eNewsletter