Local Bulletins

Matayarisho ya  siku ya wanyamapori yafanyika marsabit

Msimazi mkuu kwenye mbuga ya wanyama Marsabit national park  Augustine  Ajuoga amesema k.w.s katika kaunti ya Marsabit wanajiandaa vyema kwa siku ya kusherekea wanyama pori itakayofanyika mechi 3 mwezi ujao huku akihamasisha  jamii kujua umuhimu wa kulinda  wanyamapori pamoja na  mazingira kwa manufaa yao.

 Akizungumza na shajara ya radio Jangwani alipokuwa akifanya shughuli ya maandalizi ya siku ya kusherehekea wanyamapori duniani  ama world wildlife day   mwezi ujao ,Ajuaoga ameleezea umuhimu wa kutoa hamasisho kwa wanafunzi pamoja na jamii kwan ni jukumu na kila mmoja  kulinda wanyamapori pamoja na mazingira.

Hafla hiyo imejumuisha wanafunzi kutoka shule ya gadamoji ambapo waliweza kuzuru  mbuga hiyo ya wanyama mjini marsabit

Vile vile Augustine amesema ni jukumu la kila mwananchi  kulinda wanyama pori pamoja na mazingira haswa akiwahimiza wakaazi wa marsabit kuwa mstari wa mbele katika kulinda mazingira   kwani ina manufaa kwa jamii kwa jumla

Aidha, amesema kuwa ni sharti wakaazi wa marsabit watembelee mbuga ya wanyama huku akiwahakishia usalama wao .

Subscribe to eNewsletter