Mtu mmoja afariki kutokana na ugonjwa wa Kalazaar Marsabit, sita wakipokea matibabu kulingana na serikali ya kaunti.
February 21, 2025
Na Caroline Waforo
Raia tisa wa Ethiopia wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kuwa nchini Kenya kinyume na sheria.
Mahakama imearifiwa kuwa mnamo tarehe 15 mwezi huu wa Februari, katika mto Merille eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit raia hao tisa wa Ethiopia walikamatwa wakiwa nchini bila stakabadhi hitajika.
Tisa hao walifikishwa mahakamani leo tarehe 17 mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome ambapo walikubali kosa dhidi yao.
Walipigwa faini ya shilingi 10,000 au kifungo cha miezi 6 huku hakimu Arome akiagiza raia hao kurejeshwa makwao.