Wazazi marsabit waombwa kuruhusu watoto wao kujiunga na chama cha skauti.
February 13, 2025
Na JB Nateleng
Kuna idadi ndogo ya usajili wa wanachama wa Skauti katika kaunti ya Marsabit
Haya ni kwa mujibu wa kamishna wa wanaskauti kaunti ya Marsabit John Pope Wambisa.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya Kipekee, Pope ameelezea kuwa imekuwa ni vigumu kuwasajili wakazi wa Marsabit kwa sababu ya ukosefu wa rasilimali ya kutosha ambayo itasaidia katika kuendesha shughuli ya usajili pamoja na kutoa hamasa kwa Umma.
Pope ametoa rai kwa serekali na mashirika yasiyo ya kiserekali pamoja na watu binafsi kuweza kujitokeza na kusaidia katika kutoa hamasa kwa wakazi jimboni kuhusu umuhimu wa kuwa mwanachama wa skauti.
Aidha Pope amesema kuwa imekuwa pia vigumu kwa walimu wa kuu wa shule jimboni kuwatoza wanafunzi ada ya kujisajili kuwa wanaskauti kwa sababu ya Mawazo ya wenyeji juu ya skauti.
Hata hivo kamishna huyu amewataka wazazi kuweza kuwaruhusu wanawao kujiunga na chama cha skauti ili kujenga jamii iliyo na maadili bora.
Kadhalka Pope ameelezea kuwa lengo kuu la kuwa mwanaskauti ni kulinda na kutunza mazingira hivyo kuwarai vijana kuweza kukumbati wito huu wa kuwa wanaskauti.
wanaskauti jimboni Marsabit wanatarajiwa kusherehekea siku ya mwanzilishi wa chama cha skauti nchini jumamosi. Sherehe hiyo katika jimbo la Marsabit itaandaliwa katika shule ya upili ya Cavallera Girls.