Wazazi marsabit waombwa kuruhusu watoto wao kujiunga na chama cha skauti.
February 13, 2025
Huku dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya radio wakaazi wa Marsabit wametaja radio kuwa chombo chenye manufaa kwao kwani wanaitumia kupata habari burudani na elimu.
Wakizungumza nasi Wengi wao wametaja kupendezwa na mijadala kwenye radio inayowapa nafasi ya kuchangia na hivyo basi kupata nafasi ya mchango katika kulainisha jamii na uongozi wa nchi.
Aidha wameonyesha kuridhishwa kwao na jinsi radio haswa zilizopo maeneo ya mashinani zimekuwa zikiwapasha habari kutoka maeneo yao ya karibu kando na zile za kitaifa na kimataifa.
Mada ya mwaka huu ya siku radio ni radio na mabadiliko ya tabia nchi.
Radio kwa siku za hivi karibuni imechangia pakubwa katika kuelimisha wananchi kuhusu swala hilo la tabia nchi na vilevile kusaidia katika kuzuia athari mbaya za mabadiliko ya tabia nchi kama anavyotueleza naibu mhariri wa habari radio jangwani Samuel Kosgei.