Wazazi marsabit waombwa kuruhusu watoto wao kujiunga na chama cha skauti.
February 13, 2025
Na Moses Sabalua.
Hatua ya benki kuu nchini CBK kutaka benki za kibiashara nchini kupunguza riba ya kupeana mkopo imepongezwa na kutajwa kama njia mojawapo ya kuinua wanabiashara na biashara zao.
Mtaalam wa kifedha katika kaunti ya Marsabit John Maina amesema hatua ya Benki kuu ya Kenya kushusha riba kutoka asilimia 16.5 hadi asilimia 14 itasaidia pakubwa katika kuinua biashara na uchumi humu nchini .
Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani amesema punguzo hilo la riba litasaidia pakubwa katika kupanua biashara na itasaidia wananchi kuchukua mikopo kwa bei rahisi na itainua uchumi humu nchini pamoja na kubuni ajira kwa wananchi.