Wazazi marsabit waombwa kuruhusu watoto wao kujiunga na chama cha skauti.
February 13, 2025
NA JB NATELENG
Msitu wa Marsabit umeweza kuongezeka kwa mwaka mmoja uliopita na hili limeafikiwa baada ya ushirikiano wa idara ya misitu (KFS) pamoja na washikadau na wakazi wa Marsabit
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, msimamizi wa msitu Marsabit Kadiro Oche amesifia ushirikiano ambao umekuwepo kati ya KFS na wananchi wa Marsabit akiwataka kuzidisha bidii ya kupanda miti na kutunza kwa manufaa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kadiro amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuweza kuhakikisha kuwa ameshiriki kikamilifu katika kuboresha misitu.
Kadiro amesema kuwa idara hiyo itashirikiana na jamii zinazoishi karibu na msitu msimuu huu wa kiangazi ili kutoa ratiba ya jinsi na ambavyo watakuwa wakiwanyeshwa mifugo ama kuteka maji kwenye msitu.
Aidha Kadiro amewarai wakazi wanaoishi karibu na mizitu kuasi tabia ya kuwasha moto karibu na misitu ili kuepuka kusababisha hasara ya msitu kuchomeka.