Local Bulletins

Mwanaume mmoja auawa na ndovu katika mbuga ya wanyamapori ya Marsabit.

Na Caroline Waforo

Mwanaume mmoja wa miaka 32 ameuawa na ndovu katika mbuga ya wanyamapori ya Marsabit.

Mwanaume huyo aliyekuwa mkaazi wa Manyatta Chile ni kati ya wanaume wengine wanne waliokuwa msituni kusaka kuni bila ya idhini

Akizungumza na Radio Jangwani afisa anayesimamia wanyama pori katika kaunti ya Marsabit James Kemei amesema kuwa kisa hicho kilitokea siku ya Jumanne jioni.

Mwili wa mwanaume huyo umehifadhiwa katika makafani ya hospitali ya rufaa ya Marsabit ambapo unatarajiwa kufanyiwa upasuaji.

Kemei pia amekariri kuwa ndovu wapo pia katika eneo la Ngurunit eneobunge la Laisamis japo anasema kuwa maafisa wa shirika la KWS wako nyanjani kuhakikisha kuwa ndovu hao hawasumbui wananchi wanaoishi katika eneo hilo.

Wakaazi wa Karare, eneobunge la Saku nao wametakiwa kupiga ripoti kwa shirika la wanyapori la KWS baada ya taarifa kuibuka kuwa wanahangaishwa na Simba wawili na ambao wanasemekana kuwaua mifugo kadhaa katika eneo la karare scheme.

Haya ni huku afisa huyu wa KWS akisema kuwa mgogoro wa binadamu na wanyamapori umepungua humu jimboni Marsabit.

Aidha ametoa rai kwa wanachi kuripoti visa vyovyote vya migogoro hiyo ili kupata fidia.

Subscribe to eNewsletter