Wasichana na wanawake Marsabit watakiwa kufanya kozi ya sayansi ili kuendana soko la ajira.
February 11, 2025
NA JB NATELENG
Tume ya kuajiri walimu nchini TSC imetakiwa kuipa maslahi ya jamii kipaumbele wakati wa kufanya maamuzi ya uongozi wa shule.
Haya yamekaririwa na wazazi eneo la Kumbi Bagasa wakilalamikia kuhusu hatua ya Tume ya kuajiri walimu kutaka kumleta mwalimu mkuu aliyekataliwa na jamii ya eneo hilo katika shule ya upili ya Sasura Girls.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi pamoja na vijana wa eneo hilo, Konzo Didole Guyo ambaye ni kiongozi wa vijana amesema kuwa lazima wahusishwe kikamilifu katika kufanyaa maamuzi ya shule ya upili ya Sasura akiichangamoto kuwazia upya maamuzi yao ya ni nani anafaa kuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo.
Kadhalika jamii imemtaka mkurugenzi wa tume ya kuajiri walimu jimboni Marsabit kuweza kutembelea shule hiyo ili kuweza kuwa na kikao na wazazi badala ya kuwatuma maafisa wa tume hiyo.