Local Bulletins

Viongozi Marsabit wakosoa hatua ya serekali kuvunjilia mbali shirika la NACONNET….

NA CAROLILINE WAFORO

Serikali imeendelea kukosolewa kwa kuvunjiliwa mbali shirika la National Council for Nomadic Education NACONNET na ambalo limekuwa la manufaa makubwa kwa wakaazi wa maeneo kame ikiwemo kaunti ya Marsabit haswa katika kuinua kiwango elimu.

Wakizungumza na wanahabari leo Jumanne baadhi ya viongozi jimboni wamekosoa baraza la mawaziri kwa uamuzi huo.

Wakiongozwa na Christopher Galgallo na ambaye alikuwa mwenyekiti wa shirika hilo, viongozi hao wameonyesha masikitiko yao na sasa wamewasilisha kesi mahakamani kupinga uamuzi huo wa serikali.

Galgallo ameitaka serikali kukoma kuendesha siasa kutumia elimu ya wanafunzi haswa wa kutoka maeneo kame.

Aidha mwenyekiti huyo wa zamani wa shirika la NACONNET amemtaka Rais William Ruto kubatilisha uamuzi huo.

Naye mwakilishi wadi mteule Sadia Araru na ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya elimu katika bunge la kaunti ya Marsabit amesema kuwa uamuzi huu utakuwa na adhari kubwa haswa kwa wanafunzi wa maeneo kame.

Kauli yake ikiungwa mkono na mwasisi wa shirika la kupigania haki za kibinadamu la MWADO, Nuria Gollo ambaye ameitaka serikali kuweka wazi kilichopelekea uamuzi huo.

Majukumu ya NACONNET ni kuhakikisha kuwa inashughulikia matakwa ya wakaazi kutoka maeneo kame na ni mojawepo ya mashirika tisa ya serikali yaliyovunjwa hivi maajuzi kwa kutoiletea serikali faida.

Subscribe to eNewsletter