Local Bulletins

Hospitali ya Laisamis Level 4 yafanya upasuaji wa kwanza wa mama akijifungua mtoto….

NA ISAAC WAIHENYA

Hospitali ya Laisamis Level 4 katika kaunti ya Marsabit, inajivunia kile imekitaja kwamba ni hatua katika utoaji wa huduma baada ya kufanikiwa kufanya zoezi la upasuaji wa kwanza wakati mama anapojifungua.

Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia simu mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo Liban Wako ameitaja hatua hiyo kama ya kujivunia kwani kwa muda wamekuwa wakiwatuma wananchi wanaohitaji huduma hizo katika hospitali ya rufaa mjini Marsabit au katika kaunti jirani ya Isiolo ili kupata huduma.

Aidha Liban ameitaja hatua hiyo kama itakayoimarisha huduma za afya na kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito au hata watoto wachanga wakati wa kujifungua.

Kuhusiana na visa vya ugonjwa wa Kalazaar ambavyo viliripotiwa katika eneo bunge la Laisamis wiki jana, Liban ametaja kwamba bado kuna wagonjwa 10 ambao wamelazwa katika hospitali hiyo huku wakiendelea kupokea matibabu.

 

Subscribe to eNewsletter