Local Bulletins

Idara ya maeneo kame na ustawi miji kwa ushirikiano na NDMA yawakabidhi wakaazi wa Dadach Lakole gari la kusambaza maji maarufu (Water Bowser) ….

Na Abdiaziz Yusuf,

dara ya maeneo kame na ustawi miji kwa ushirikiano na mamlaka ya kupambana na majanga NDMA hii leo imekabidhi gari la kusambaza maji maarufu (water bowser) kwa wakaazi wa dadach lakole wadi ya Butiye katika juhudi za kupambana na kero la ukosefu wa maji katika eneo hilo.

Akizungumza wakati wa hafala hiyo katibu katika idara ya maeneo kame na ustawi miji Kello Harsama amesema kuwa hatua hiyo inatokana na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji haswa wakati wa ukame.

Aidha katibu Kello amesema kuwa gari hilo litasaidia jamii na kuboresha maisha ya kimsingi.

Hata hivyo wakaazi wa eneo hilo wamepokea masaada huo kwa furaha na kuishukuru serekali kwani utawasaidia kupunguza shughuli za kutembea mbali kutafuta maji.

Hata hivyo wameyataka mashirika yasiyoyakjkiserekali jimboni Marsabit kwa ushirikiano na serekali kuzidi kuwapiga jeki haswa kipindi hichi cha kiangazi.

Subscribe to eNewsletter