Local Bulletins

Wakenya watakiwa kujitokeza kwa uchunguzi wa ugoinjwa wa saratani mapema…..

Na Isaac Waihenya,

Wakaazi hapa nchini wametakiwa kujitokeza kwa uchunguzi wa ugoinjwa wa saratani mapema.

Wito huu umetolewa na afisa mkurugenzi mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Eldoret daktari Philip Kirwa.

Akizungumza hii leo wakati wa maadhimisho ya siku ya saratani dunia Kirwa amehimiza haja ya watu kujitokeza kwa uchunguzi wa saratani mapema ili waweza kuanza matibabu huku akiwahimiza haja ya wagonjw akukumbatia matibabu ya kisasa.

Aidha Kirwa ameongeza kuwa baadhi ya watu wanageukia tiba ya kiasili wanapogunduliwa kuwa wana ugonjwa wa saratani baada ya kuendelea na matibabu hospitali ili waweza kupokea matibabu ya mapema.

Hata hivyo Kirwa amefichua kuwa hospitali hiyo hupokea wangojwa wapya elfu 6,000 wanaopatikana na ungojwa wa saratani kila mwezi.

Amesema kuwa mia sita kati yao huendelea kupokea mnatibabu katika hospitali hiyo kila mwezi huku akikiri kuwa wengi wao hufika hospitali wakati ugonjwa huo umesonga sana.

Subscribe to eNewsletter