Kero la uhaba wa maji katika kata ya Golole,Moyale, lapata suluhu,baada ya kisima cha Golole 3 kuzinduliwa hii leo.
February 3, 2025
Na Abdiaziz Yusuf,
Hatimaye kero la uhaba wa maji katika kata ya Golole wadi ya Uran eneo Bunge la Moyale limepata suluhu. Hii ni baada katibu wa kudumu katika idara ya maeneo kame na ustawi wa miji Kello Harsama kwa ushirikiano wa kerikali kuu kupitia mamlaka ya kushughilikia majanga nchini NDMA kuzindua rasmi kisima cha Golole 3 hii leo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kisima hicho Katibu Kello mesema kuwa ufanisi huo umeafikiwa kutokana na ushirikiano dhabiti kati ya idara yake ya mamlaka ya kushughilikia majanga nchini NDMA.
Aidha katibu Kello ameweka wazi kuwa mradi huo umegarimu shillingi milioni 15 na utnufaisha zaidi ya kaya 500 katika eneo hilo.
Kwa upande wake mratibu wa mmlaka ya NDMA katika kaunti ya Marsbit Guyo Golicha amewataka wakazi wa Golole kuchunga kisima hicho ili kiweze kuwanufaisha kwa kipindi kirefu.
Wakati uo huo Dabaso Dambi kwa niaba ya wakazi wa Golole amesema kuwa wamenufaika na kisima hicho na kutoa shukrani zake kwa idara ya maeneo kame na ustawi wa miji pamoja na NDMA kwa kutekeleza mradu huo.