Kero la uhaba wa maji katika kata ya Golole,Moyale, lapata suluhu,baada ya kisima cha Golole 3 kuzinduliwa hii leo.
February 3, 2025
Na JB Nateleng,
Wito umetolewa kwa idara ya maji kaunti ya Marsabit kuweza kukarabati kisima cha Boqe kilichopo lokesheni ya Kalacha eneo bunge la North horr.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu, chifu wa eneo la Kalacha Sabdio Wario amesema kuwa kisima hicho kiliharibika mnamo mwaka wa 2021 na mpaka sasa hivi hakujakuwa na mpango wa kukarabati huku wakaazi wakiendelea kutaabika kutokana na uhaba wa maji.
Sabdio ameelezea kuwa shughuli za masomo pia zinaweza kutatizika katika eneo hilo kwa sababu ya uhaba wa maji huku akitoa wito kwa swala hilo kuangaziwa kwa kina na kupewa kipaumbele.
Vile vile Sabdio amesema kuwa kupitia ufadhili kutoka kwa wahisani eneo hilo liliweza kupewa lori nne za kusambaza maji mashinani japo bado mahitaji ni mengi.
Kadhalika ameirai serekali ya kaunti kupitia idara ya maji kuweza kutengeneza kisima cha Boqe ili kurahisisha upatikanaji wa maji kwa wakazi wa eneo hilo.